Job awatoa hofu mashabiki wa Yanga
Juzi katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya Afcon 2025 ambapo Tanzania ilikuwa ugenini kukabiliana na Guinea, beki Dickson Job alizua hofu kwa Wananchi baada ya kupata majeraha ambayo yalimfanya ashindwe kuendelea na mchezo ikiwa ni dakika ya 9
Job alipata maumivu ya kichwa baada ya kugongana na mchezaji wa Guinea, alipatiwa msaada na madaktari kabla ya kutolewa nje nafasi yake ikichukuliwa na Bakari Nondo Mwamnyeto
Job amewatoa hofu Wananchi kuwa yuko sawa kiafya tayari kuitumikia Yanga katika mchezo dhidi ya CBE siku ya Jumamosi
"Nilipata changamoto ambayo ilinifanya nishindwe kuendelea na mchezo baada ya kugongana na mchezaji wa Guinea hadi kupelekea kuathiri uwezo wangu wa kuona kwa muda"
"Lakini sasa naona vizuri, mashabiki wasiwe na wasiwasi nitarudi kazini kwenye majukumu yangu, hadi sasa ninavyojisikia naona nitaweza kuwa sehemu ya timu kwenye mechi inayofuata kule Addis Ababa," alisema
Yanga iliondoka nchini mapema leo ikiwa na wachezaji ambao hawakuwa na majukumu ya timu za Taifa. Wataungana na wenzao Addis Ababa
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Post a Comment