Gamondi amepata dawa ya wanaopaki basi
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amelazimika kurudi katika uwanja wa mazoezi ili kuboresha mbinu zake ili kukabiliana na timu 'zinazopaki basi'
Juzi baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KenGold, maafisa wa timu hiyo walionekana kufurahia kufungwa bao 1 tu na kumpongeza kocha wao kwa mbinu zilizowasaidia kupunguza idadi ya mabao
Katika moja ya mahojiano yake, Gamondi alisema anafahamu kila timu watakayokutana nayo kwenye ligi msimu huu, itaweka watu wengi nyuma kutafuta sare au kupunguza idadi ya mabao kwani kufungwa mabao machache na Yanga kwa wengine ni mafanikio
"Ni lazima tujipange upya ili kuwa na machaguo ya mbinu za kutengeneza mabao hata kama tunakutana na timu zinazokaa nyuma"
"Kwenye mazoezi yetu tumeanza kujipanga na hilo kuhakikisha tunakuwa tayari kukabiliana na ugumu wa namna hiyo"
"Mabeki wa pembeni, viungo na hata washambuliaji wanapaswa kuwa na njia nyingi za kutengeneza nafasi na hata kutumia nafasi ambazo watakazopata," alisema Gamondi
Yanga imedhamiria kutetea ubingwa wake kwa msimu wa nne mfululizo, inahitaji kukusanya alama nyingi na kufunga mabao mengi
Katika mechi mbili za kwanza Yanga imeshinda zote na kufunga mabao matatu, ikiwa nafasi ya 7 katika msimamo
Wananchi wana deni la mabao sita dhidi ya watani zao Simba ambao wamefunga mabao 9 katika mechi tatu
Kazi ya kusaka pointi na mabao inaanza Jumapili hii ya kufosi katika mchezo dhidi ya KMC
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Post a Comment