CBE wameandaliwa dozi New Amaan Complex - EDUSPORTSTZ

Latest

CBE wameandaliwa dozi New Amaan Complex

CBE wameandaliwa dozi New Amaan Complex


Usikose kuitazama mechi ya YANGA vs CBE Live bure kwenye simu yako download app yetu itakayo kuwezesha kuitazama mechi hii bure kabisa pia ukiwa na app yetu utweza kutazama chanel za AZAM TV na DSTV bure kabisa pia na mechi zote za Nbc premier league na mechi zote za Ulaya kudownload app yetu bonyeza 👉🏻HAPA


 Jumamosi Septemba 21 Yanga inakwenda kukamilisha mchezo wa mkondo wa pili kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya CBE SA

Kikosi cha kocha Miguel Gamondi kitaingia katika mchezo huo kikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza

Kimahesabu Yanga inahitaji ushindi au matokeo yoyote ya sare ili kutinga hatua ya makundi

Lakini matarajio ya mashabiki wa Yanga ni kuona timu yao inaibuka na ushindi mnono zaidi katika dimba la New Amaan Complex

Yanga ina rekodi nzuri ya kufunga mabao msimu huu ambapo mpaka sasa imepachika mabao 18 katika mechi za mashindano

Washambuliaji Prince Dube na Clement Mzize watakuwa na nafasi ya kuendeleza kasi yao ya kufunga kila mmoja akiwa amepachika mabao manne

MVP wa ligi kuu msimu uliopita Stephane Aziz Ki mpaka sasa amefunga mabao matatu huku Clatous Chama na Maxi Nzengeli kila mmoja akifunga mabao 2

Pacome Zouzoua na Mudathir Yahya nao ni miongoni mwa wachezaji waliopachika mabao ambapo kila mmoja amefunga bao 1

CBE SA walinusurika na kipigo kizito katika uwanja wao wa nyumbani kwani licha ya kufungwa bao 1 tu, Yanga ilipoteza takribani nafasi saba

Pengine Jumamosi wanaweza kukumbana na kile kilichowakuta Vital'o kama hawatakuwa makini

KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA


PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE  HAPA



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz