Beki wa kazi Simba atoweka kambini - EDUSPORTSTZ

Latest

Beki wa kazi Simba atoweka kambini

Beki wa kazi Simba atoweka kambini

Usikose kuitazama mechi ya AZAM FC vs SIMBA Live bure kwenye simu yako download app yetu itakayo kuwezesha kuitazama mechi hii bure kabisa pia ukiwa na app yetu utweza kutazama chanel za AZAM TV na DSTV bure kabisa pia na mechi zote za Nbc premier league na mechi zote za Ulaya kudownload app yetu bonyeza 👉🏻HAPA

Aisha Mnunka.

Wakati sakata la mshambuliaji wa Simba Queens, Aisha Mnunka likiwa bado halijaisha, limejibuka jipya kuhusu beki wa timu hiyo Mkongomani Daniella Ngoyi ambaye naye haonekani klabuni na hajatoa taarifa.

Daniella anakuwa mchezaji wa pili kuondoka kambini bila taarifa baada ya awali Aisha ambaye tangu Simba Queens itangaze hawamuoni, bado hajatokea kikosini hapo.

Simba Queens ipo Bunju jijini Dar es Salaam ikijifua kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL)inayotarajiwa kuanza mwezi ujao.

Kabla ya kuingia kambini wiki iliyopita, Simba Queens ilitoa mapumziko ya wiki moja kwa wachezaji baada ya kutoka kwenye michuano ya Cecafa, huku beki huyo ikidaiwa hajajiunga na wenzake.

Taarifa za ndani ya Simba zinaeleza nahodha huyo wa timu ya taifa ya wanawake ya DR Congo, amebeba kila kitu chake kilikuwepo kambini na viongozi hawana taarifa yoyote juu ya kuondoka kwake.

“Viongozi wamewasiliana naye karibu wiki sasa lakini simu haipatikani na hata watu wake wa karibu hawajui alipo,” ilisema taarifa hiyo. Mtu wa karibu na nyota huyo, ameliambia Mwanaspoti kwamba: “Aliniaga anakwenda Congo akiahidi atarudi, sasa sijajua hayo mengine licha ya kwamba muda mrefu umepita.”

Alipotafutwa Meneja wa Simba Queens, Seleman Makanya ili kuzungumzia sakata hilo, simu yake ya mkononi iliita bila ya kupokelewa. Hii sio mara ya kwanza kwa mchezaji huyo kutoonekana kambini kwani iliwahi kutokea mwaka 2022 akiwa na Yanga Princess kabla ya kuibukia Simba Queens msimu wa 2022-2023.

KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA


PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE  HAPA



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz