Baada ya timu ya Simba kufanyiwa vurugu jana Ahmed Ali atoa kauli hii - EDUSPORTSTZ

Latest

Baada ya timu ya Simba kufanyiwa vurugu jana Ahmed Ali atoa kauli hii

Baada ya timu ya Simba kufanyiwa vurugu jana Ahmed Ali atoa kauli hii

Usikose kuitazama mechi ya YANGA vs CBE Live bure kwenye simu yako download app yetu itakayo kuwezesha kuitazama mechi hii bure kabisa pia ukiwa na app yetu utweza kutazama chanel za AZAM TV na DSTV bure kabisa pia na mechi zote za Nbc premier league na mechi zote za Ulaya kudownload app yetu bonyeza 👉🏻HAPA

 Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuwa timu yao iko salama licha ya 'purukushani' zilizojitokeza uwanjani baada ya mchezo dhidi ya Al Ahly Tripoli uliopigwa jana huko Libya

Baada ya mchezo huo uliomalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana, mashabiki wa Al Ahly Tripoli walifanya vurugu uwanjani kwa kuwarushia chupa wachezaji wa Simba pamoja na waamuzi

Ahmed amesema timu ililazimika kukaa uwanjani kwa takribani dakika 40 kabla ya kupanda basi kuelekea hotelini

"Tunashukuru tuko salama pamoja na vurugu zilizojitokeza, tumerejea hotelini salama kabisa"

"Baada ya mchezo kumalizika vurugu zilijitokeza uwanjani, maafisa usalama walitushauri tuende vyumbani tusubiri mashabiki waondoke uwanjani ndipo nasi tuondoke"

"Hivyo tulikaa uwanjani kama dakika 40 ndipo tukapanda basi kuelekea hotelini. Kulikuwa na tukio la golikipa wetu Aishi Manula kushambuliwa wakati tunatoka jukwaani kuelekea katika vyumba vya kubadilishia nguo, lakini tunashukuru nae hakupata madhara yoyote"

"Manula alishambuliwa na moja ya maafisa wa usalama katika tukio la kushangaza kwani ni wao waliotushauri tuende katika vyumba vya kubadilishia nguo tusubiri vurugu zutulie," alisema Ahmed

Simba inatarajiwa kuondoka leo kurejea Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano ambao utapigwwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Jumapili ijayo

KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA


PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE  HAPA



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz