Wapinzani wa Simba washtuka, washusha ‘bodyguards’ kibao Airport - EDUSPORTSTZ

Latest

Wapinzani wa Simba washtuka, washusha ‘bodyguards’ kibao Airport

Al Ahli Tripoli wawasili Dar na Mabodigadi wao
Unaanzaje kukosa burudani hii Usikose kuitazama mechi ya SIMBA vs AL AHLI TRIPOLI Live bure kwenye simu yako download app yetu itakayo kuwezesha kuitazama mechi hii bure kabisa pia ukiwa na app yetu utweza kutazama chanel za AZAM TV na DSTV bure kabisa pia na mechi zote za Nbc premier league na mechi zote za Ulaya kudownload app yetu bonyeza 👉🏻HAPA
Wapinzani wa Simba washtuka, washusha ‘bodyguards’ kibao Airport

Katika hali isiyo ya kawaida, wapinzani wa Simba, Al Ahli Tripoli wamekodi walinzi binafsi ‘bodyguards’ kwa ajili ya kuwalinda wachezaji pamoja na benchi la ufundi pindi kikosi kitakapotua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Al Ahli Tripoli inatarajiwa kuwasili Dar es Salaam saa tatu asubuhi ya leo kwa ajili ya kucheza mchezo wa marudiano kutafuta tiketi ya kufuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Simba.

Mchezo huo utachezwa Jumapili ya wiki hii Septemba 22, 2024 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam baada ya ule wa awali nchini Libya kumalizika kwa matokeo ya 0-0.

Mmoja kati ya watu waliokuja kuwapokea ambaye hakutaka jina lake kuandikwa, ameliambia Mwanaspoti kuwa wameandaa ulinzi huo kwani wanahofia kufanyiwa fujo.

“Jamaa wanaogopa kutokana na yaliyotokea kule kwao, hata hapa tulipo hatujaambiwa wanafikia hoteli gani, hadi wafike ndio tutajua,” alisema mtu huyo.

Ikumbukwe kwamba, baada ya mchezo wa wikiendi iliyopita uliochezwa nchini Libya na timu hizo kushindwa kufungana, iliripotiwa mashabiki wa Al Ahli Tripoli waliwafanyia fujo wachezaji wa Simba wakati wanarudi vyumbani. Pia ilielezwa wachezaji wa timu hiyo na viongozi waliwashambulia waamuzi.

Mbali na hilo, kipa wa Simba, Aishi Manula iliripotiwa alipigwa na ofisa mmoja aliyekuwa akiimarisha usalama uwanjani.


KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA


PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE  HAPA



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz