Yanga yakomba tuzo saba usiku wa TFF
Usikose kutazama sherehe za Simba Day Live bure kupitia simu yako download app yetu mapema ili usipitwe na tukio hili maalumu la Simba Day pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel zote za Azam tv na Dstv bureee download sasa app yetu kudownload App yetu bonyeza 👉🏻HAPA
Jana tuzo za TFF katika ligi kuu na kombe la FA ilibaki kidogo ziwe 'sold out' mikononi mwa Wananchi
Yanga ilikomba tuzo saba katika usiku wa tuzo za TFF huku nyota sita wakiingia katika kikosi bora cha msimu
Stephane Aziz Ki alikuwa kinara kwa kukomba tuzo nyingi, akibeba tuzo nne ambazo ni MVP, kiungo bora, mfungaji bora na kikosi cha msimu
Ibrahim Bacca akabeba tuzo mbili, beki bora na kikosi cha msimu
Kocha Miguel Gamondi akabeba tuzo ya kocha bora huku Clement Mzize akibeba tuzo ya mfungaji bora kombe la FA, Djigui Diarra akibeba tuzo ya kipa bora FA
Nyota walioingia katika kikosi bora cha msimu ni Yao Kouassi, Ibrahim Bacca, Aziz Ki, Mudathir Yahya, Maxi Nzengeli na Dickson Job
Post a Comment