TFF yaionya Simba SC
Usikose kuitazama mechi ya VITALO FC vs YANGA kesho kutwa miachuano ya Caf champions league LIVE bure kupitia simu yako download app yetu itakayokuwezesha kuitazama mechi hii bure kabisa pia ukiwa na app yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure download sasa app yetu kuidownload bonyeza 👉🏻HAPA
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetoa onyo kwa Simba SC kwa kumrubuni mchezaji wa KMC Fc Awesu Awesu na kumtangaza kuwa mchezaji wao katika mitandano yake ya kijamii bila kufuata utaratibu.
Taarifa ya TFF imefafanua kuwa uamuzi huo umefikiwa katika kikao chake cha tarehe Agosti 10, 2024 ikasikiliza pande zote mbili (KMC FC na Simba SC) kabla ya kuamua kuwa Awesu Ali Awesu ni mchezaji halali wa KMC FC, na kama Simba SC inamuhitaji mchezaji huyo izungumze na klabu yake.
“Malalamiko ya klabu yako ni kuwa Simba SC imemrubuni mchezaji Awesu Ali Awesu, na kumtangaza kuwa mchezaji wao katika mitandano yake ya kijamii bila kufuata utaratibu wakati suala lake likiwa bado halijatatuliwa.”
Hata hivyo Kamati ya TFF imekiri kuwa haikupata ushahidi wowote kutoka KMC Fc kuwa Simba Sc ilimrubuni mchezaji huyo wa zamani wa Madini Fc.
Post a Comment