Huyu hapa Pilato Fainali Ngao ya Jamii - EDUSPORTSTZ

Latest

Huyu hapa Pilato Fainali Ngao ya Jamii

Huyu hapa Pilato Fainali Ngao ya Jamii

Usikose kuitazama Fainali ya ngao ya Jamii kati ya YANGA vs AZAM FC Live bure kupitia simu yako download app yetu kutazama mechi hii bure kabisa pia ukiwa na app yetu utaweza kutazama chanel za Azam Tv na Dstv live bure kudownload app yetu bonyeza 👉🏻HAPA

Ahmed Arajiga

Mwamuzi Ahmed Arajiga kutoka Manyara, ameteuliwa kuchezesha fainali ya Ngao ya jamii kati ya Yanga dhidi ya Azam utakaopigwa kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 usiku.

Yanga imepata tiketi hiyo baada ya kuwaondoa Simba kwa kuichapa bao 1-0, huku Azam wakishinda 5-2 dhidi ya Coastal Union.

Arajiga ambaye alichezesha nusu fainali ya kwanza ya Ngao ya Jamii kati ya Azam dhidi ya Coastal, atasaidiwa na Frank Komba kutoka Dar es Salaam na Mohammed Mkono wa Tanga.

Mkono anarudi tena kwenye mchezo huu baada ya kuwepo katika nusu fainali ya pili ya Ngao ya Jamii ambayo Yanga iliichapa Simba akiwa mwamuzi msaidizi namba moja.

Amina Kyando wa Morogoro atakuwa mwamuzi wa akiba kwenye mchezo huo huku Soud Abdi (Arusha) akipewa jukumu la kuwatathimini waamuzi hao. Hawa nao walikuwepo katika mchezo wa Yanga dhidi ya Simba kwenye majukumu yao hayohayo.

Naye mwamuzi Ramadhan Kayoko wa Dar es Salaam amepewa jukumu la kuamua mchezo kati ya Simba na Coastal Union wa kusaka nafasi ya tatu katika Ngao ya Jamii.

Mchezo huo utakaoanza saa 9:00 alasiri kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Kayoko ataisaidiwa na Glory Tesha atakayekuwa mwamuzi msaidizi namba moja, Hamdan Said ni mwamuzi msaidizi namba mbili, wakati Isihaka Mwalile (Dar es Salaam) akiwa mwamuzi wa akiba huku Issaro Chacha (Mwanza) atakuwa mtathimini wa waamuzi.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz