Hakuna timu dhaifu ligi ya mabingwa - Kamwe

Hakuna timu dhaifu ligi ya mabingwa - Kamwe

USikose kuitazama mechi ya VITALO vs YANGA pia na SIMBA vs TABORA UNITED live bure kupitia simu yako download app yetu kuzitazama mechi zote bure pia ndani ya app yetu utaweza kutazama na mechi za ulaya live bure kudownload app yetu bonyeza 👉🏻HAPA

 Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema wameuchukulia mchezo dhidi ya Vital'o kwa umakini mkubwa kwani wanatambua hakuna timu ndogo katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Kesho Jumamosi, Yanga itakuwa ugenini uwanja wa Azam Complex kuikabili Vital'o katika mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali

Kamwe amesema hawataidharau timu yoyote watakayokutana nayo kwa sababu anaamini hakuna timu dhaifu inayocheza mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika

"Ndugu zanguni hakuna timu dhaifu inayocheza Ligi ya Mabingwa Afrika, zote ni ngumu na zote ni mabingwa kwenye nchi zao, kwa hiyo, hatuidharau Vital'o wala hatutakwenda kucheza kwa dharau, tunachohitaji ni kwenda kupambana, ikiwezekana tupate mabao mengi," alisema Kamwe

Aidha Kamwe amesema wamezisikia tambo za klabu ya Vital'o kuelekea mchezo huo lakini wao kauli yao ni moja tu, 'tukutane uwanja wa Azam Complex Jumamosi'

Naye Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema atahitaji kuona vijana wake wanaongeza umakini katika mchezo huo kwani malengo ni kuona wanashinda na kusonga mbele hatua inayofuata

Afisa Habari wa Vital'O ametamba kuwa Yanga isitarajie ushindi kirahisi kwa sababu wao pia wamejipanga kisawasawa kuhakikisha wanapata matokeo mazuri

"Wengi wanatuona kama wepesi tu, kwa sababu tumecheza na Pamba Jiji tumetoa sare tena tumesawazisha bao mwishoni, lakini hawajui kila mechi ina mbinu zake, wachezaji wa Pamba ni wazuri, pia hatuwajui kwa sababu hatujawahi kuona video zao, lakini Yanga tunaziona na tunazifanyia kazi," alisema


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post