Gamondi: Sijaridhika na matokeo ya kwanza dhidi ya Vital'O, kesho watakula nyingi - EDUSPORTSTZ

Latest

Gamondi: Sijaridhika na matokeo ya kwanza dhidi ya Vital'O, kesho watakula nyingi

Gamondi: Sijaridhika na matokeo ya kwanza dhidi ya Vital'O, kesho watakula nyingi

Usikose kuitazama mechi ya YANGA vs VITALO FC kesho live bure kupitia simu yako download app yetu itakayokuwezesha kuitazama mechi hii live bure pia ndani ya app yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na DSTV bure kudownload app yetu bonyeza 👉🏻HAPA

Kikosi cha Yanga.

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa anategemea kufanya mabadiliko kwenye kikosi chake cha kesho dhidi ya Vital'O ya Burundi ili kuruhusu wachezaji wengine kupata nafasi kwenye mchezo huo utakaopigwa kwatika Dimba la Azam Complex.

Gamondi amesema ana kikosi kipana chenye wachezaji wengi bora lakini hilo halimfanyi akawadharau Vital'O licha ya kuwafunga bao 4-0 kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya awali CAFCL.

“Tuko sawa, tumekuwa na mazoezi mazuri wiki nzima, tumejiandaa kwa ubora kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye mchezo wetu wa kesho na tunaamini tutapata matokeo mazuri na kusonga mbele kwenye hatua inayofuata.

“Kwenye soka huwezi kutabiri matokeo mpaka kipenga cha mwisho cha mwamuzi. Lakini ni kweli kwamba matokeo ya mchezo uliopita yametupa nguvu na utulivu zaidi, akili yetu tumeielekeza kwenye mchezo huo na wala hatujaridhika na matokeo ya mchezo wa kwanza. Tutapambana kwa asilimia 100 mbele ya mashabiki wetu ili tuweze kushinda mchezo huo.

“Kuna mabadiliko machache tutayafanya kwenye mchezo wa kesho kwa sababu tuna wachezaji wengi wenye ubora, tuna mchezo mwingine wa ligi Alhamisi tunahitaji ku-manage hili lakini malengo yetu ya kwanza ni kwa sasa ni kusonga mbele kwenye hatua inayofuata ya michuano ya CAF. Nitajitahidi kupanga kikosi bora lakini kutakuwa na mabadiliko,” amesema Gamondi.

KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA


PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE  HAPA



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz