Aishi Manula apewa 'thank you' Simba

Aishi Manula apewa 'thank you' Simba

Ni kesho kutwa Usikose kuitazama mechi ya SIMBA vs YANGA Live bure kupitia simu yako download app yetu mapema ili usipitwe na mechi hii live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel zote za Azam tv na Dstv bureee download sasa app yetu kudownload App yetu bonyeza 👉🏻HAPA

Aishi Manula

Aliyekuwa kipa namba moja wa Simba, Ashi Manula ametemwa kwenye kikosi cha timu hiyo kwa msimu ujao wa 2024/25 baada ya timu hiyo kutambulisha makipa wanne huku jina lake likiondolewa.

Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally ndiye alikuwa anataja majina ya mastaa wa kikosi hicho msimu ujao katika tamasha la Simba Day linalofanyika Uwanja wa Mkapa, ambapo ametaja majina manne eneo la makipa.

Makipa hao ni Ally Salim, Ayoub Lakred, Mohammed Camara na Hussein Abel ndiyo idadi ya walinda lango  watakaoiongoza Simba eneo la golini.

Wakati wa kutaja majina hayo nyomi ya mashabiki iliyojaza uwanja iliibua shangwe baada ya kusikia jina la Lakred ambaye inaelezwa kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita kutokana na kuumia akiwa mazoezini.

Pia shangwe kubwa limeibuka baada ya kutajwa kwa kipa mpya wa timu hiyo ambaye amesajiliwa kwa lengo la kuziba pengo la Lakred ambaye atakuwa nje ya uwanja kwa muda akiuguza jeraha alilolipata.

“Hawa ndio walinda mlango ambao tutakuwa nao msimu ujao,” amesema Ahmed.

Anaandika Meneja wa nyanda wa Simba Sc, Aishi Manula, Jemedari Said Kazumari

“TUMESIKITIKA NA TUNAJIANDAA KULIPELEKA SUALA HILI MBELE YA MAMLAKA ZA MPIRA NDANI NA NJE YA NCHI. Tunazungumza na wanasheria wetu kuona namna watakavyoshughulia suala la klabu ya Simba na mchezaji wetu AISHI MANULA kwa kitendo cha Simba KUMZUIA mchezaji kucheza soka ambacho kinapingana na kanuni za FIFA. Mchezaji haumwi wala hana jeraha lolote, hajawahi kupewa taarifa yoyote na klabu yake ambayo ana mkataba nayo kwa mwaka 1, kuhusiana na chochote cha klabu.

Hajawahi kuambiwa kupima afya kwahiyo hajapima afya kama wengine, hajashirikishwa kwa namna yoyote kwenye mazoezi ya Misri mpaka timu imerudi hajaambiwa lolote na leo Simba imetangaza kikosi chake yeye hajatajwa popote mpaka Meneja wake alipolalamika ndiyo jina lake likatajwa.

Alipata timu ambayo iliandika barua kumuomba mchezaji lakini Simba wamekataa, wao hawamtaki na kumuacha aondoke akacheze hawataki pia, mchezaji maisha yake ni mpira na Simba wanamzuia mchezaji kucheza mpira, wanasheria watatuambia kanuni za FIFA zinasemaje na zile za TFF, zinaruhusu uhuni wa namna hii?

Mwisho Simba kama klabu inatoa meseji gani kwa wachezaji wengine? HAIKUBALIKI..!!”

KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA


PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE  HAPA

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post