Baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Augsburg katika michuano ya Mpumalanga Premier's International Cup, Yanga leo inashuka tena dimbani kumenyana na TS Galaxy katika mchezo wa pili ambao utahitimisha ushiriki wa Yanga katika michuano hiyo maalum ya pre-season
TS Galaxy inashiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini ambapo msimu uliopita ilimaliza katika nafas ya 6
Akizungumzia maandalizi ya Yanga kuelekea mchezo huo utakaopigwa saa 10 jioni, Meneja wa Yanga Walter Harrison amesema ni mchezaji mmoja tu ambaye atakosekana lakini wengine wote wako tayari
"Tumejiandaa vyema kwa ajili ya mchezo huu, ukimuondoa Chadrack Boka ambaye alipata changamoto katika mchezo uliopita, wengine wote wako tayari na wanaweza kutumika katika mchezo huo," alisema Walter
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi anatarajiwa kuwapa nafasi wachezaji wote katika mchezo huo hivyo tutarajie mabadiliko ya kikosi kwenye kila kipindi
App yetu itarusha mchezo huo 'mbashara 'kuanzia saa 10 jioni (saa 9 Afrika Kusini)
Post a Comment