Supu kama kawaida Jangwani Jumamosi
Yanga ilizindua rasmi wiki ya Wananchi juzi Jumatatu ambapo leo Wananchi watashiriki matukio ya usafi na kutembelea wagonjwa Hospitalini
Kwa hapa jijini Dar es salaam, Wananchi wanafanya usafi na kutembelea Hospitali ya Temeke
Kesho Alhamisi kutakuwa na zoezi la kuchangia damu nchi nzima ambapo Wananchi watachangia damu katika maeneo yao
Ijumaa itafanyika dua maalum ya kuwaombea watu wote waliotangulia mbele za haki, kuiombea timu, wachezaji, viongozi na mashabiki
Tukio kubwa litajiri Jumamosi Makao Makuu ya Yanga pale Jangwani ambapo Wananchi watakutana mapema asubuhi kwa ajili ya 'jogging' itakayofuatiwa nasupu
Sportpesa wamedhamini supu ya Wananchi ambapo zaidi ya n'gombe 20 wametolewa kwa ajili ya tukio hilo
Jumapili Yanga itahitimisha wiki ya Wananchi kwa burudani kubwa pale uwanja wa Benjamin Mkapa
Hii itakuwa siku ya burudani kuanzia asubuhi ambapo itahitimishwa na mchezo kati ya Yanga dhidi ya Red Arrows ya Zambia
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Post a Comment