Simba yaweka ngumu kwa Kibu
Baada ya kuondoka bila ya ruhusa ya uongozi na kutimkia Ulaya, klabu ya Simba imezuia usajili wa winga Kibu Denis kujiunga na Kristiansund BK ya Norway, imefahamika
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Simba imethibitisha kuwa Wekundu hao wa Msimbazi wako tayari kumuuza Kibu kwenda Kristiansund BK lakini kwa sharti la mchakato huo kufanyika Kibu akiwa nchini
Simba imegoma kutoa baraka zake kwa mchezaji huyo kuitumikia Kristiansund BK na hivyo kuilazimu timu hiyo kuachana na mchakato wa kumsajili hadi pale atakapomalizana na Simba
Aidha kitendo alichofanya Kibu kutojiunga na kambi Misri na kutorokea Ulaya wakati uongozi ukifanya jitihada za kumpeleka Misri, kimewakera mabosi wa Simba na pengine kuna uwezekano mkubwa hatakuwa sehemu ya kikosi msimu ujao
Simba itakuwa tayari kumuuza kwenda Norway kama atatii agizo la kurejea nchini lakini kama hatatii ni wazi hataweza kusajiliwa na timu yoyote mpaka pale mkataba wake utakapomalizika 2026
Lakini pia atakuwa hatarini kukumbana na rungu la FIFA kwa kosa la kuvunja mkataba kinyume cha utaratibu kama ataendelea kosekana kutumikia mkataba wake na Simba
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Post a Comment