Simba yatua kwa Awesu
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Simba ni kuwa Wekundu hao wa Msimbazi huenda wakafunga usajili wa ndani na kiungo Awesu Awesu aliyeitumikia KMC msimu uliopita
Awesu alikuwa na msimu bora katika kikosi cha KMC msimu uliopita nyota huyo wa zamani wa Azam Fc akiwa mahodha wa timu hiyo
Simba imeongeza mafundi zaidi katika eneo la kiungo, Awesu ni 'technician' ambaye hazungumzwi sana kwa sababu hachezi timu kubwa lakini kama atatua Simba wengi watapata fursa ya kutambua ubora wake
Aidha Simba bado haijamtambulisha kiungo Yusuph Kagoma ambaye inaelezwa ana changamoto katika usajili wake
Simba 'ilimpora' Kagoma mikononi mwa Yanga ambapo licha ya mchezaji huyo kuchukua pesa ya usajili Yanga, akavutiwa na ofa nono zaidi iliyotolewa na Simba na hivyo kukubali kusani mkataba huku akiwa pia amesaini mkataba wa awali na Yanga
Mchezaji huyo alikuwa tayari kurejesha fedha zote alizopewa na Yanga ila changamoto ni kwa kuwa anakwenda kujiunga na Simba
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Post a Comment