Kibu haidai Simba - Ahmed
Usikose kuitazama mechi ya YANGA vs TS GALAXY FC michuano ya Mpumalanga cup Live hapa bure
Ni kesho saa 10: 0 jioni usikose kuitazama mechi hii LIVE bure kupitia simu yako download app yetu mapema ili uweze kuitazama mechi hii kudownload app yetu bonyeza 👉🏻HAPA
Meneja wa Habari na Mwasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amesema kiungo mshambuliaji Kibu Denis amelipwa fedha zake zote za usajili na ndio maana aliongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia Simba
Ahmed amesema uongozi unashughulikia suala lake ili ajiunge na wenzake Misri lakini mpaka sasa hajatuma hati yake ya kusafiria kama alivyoagizwa
"Simba tayari imeshamlipa Kibu Denis pesa zake zote na amesaini mkataba wa miaka 2 na Klabu yetu. Hakuna anachotudai kwa sasa ndiyo maana tunashughulikia uwezekano wa mchezaji kujiunga na wenzake kambini Misri
"Kwa taarifa niliyokuwa nayo tayari tumeshamwambia atutumie passport yake ili tuweze kufanya tratibu za kumkatia Visa ili aweze kujiunga na wenzake kambini huko Misri ila mpaka sasa bado hajatutumia," alisema Ahmed
Wakati Ahmed akitoa taarifa hiyo, kuna kila dalili huenda Kibu asisafiri kwenda Misri badala yake akaungana na timu pale itakaporejea nchini
Simba iko katika wiki ya mwisho la pre-season ambapo Kocha Mkuu Fadlu Davis jana alisema wako katika program za kuhitimisha kambi yao hapo Misri na pengine huenda Simba ikarejea nchini mwishoni mwa wiki
Kwa muda uliobaki Kibu anaweza kufanya mazoezi ya siku mbili tu au tatu jambo ambalo naamini Simba haiwezi kutumia gharama kumsafirisha Misri kwa ajili ya mazoezi ya siku mbili
Lakini pia kuna taarifa kutoka ndani ya uongozi kuwa Kibu atakatwa mshahara kwa kitendo cha kushindwa kushiriki pre-season na wenzake huku taarifa za ndani zikidokeza kuwa Kibu amepata ofa kutoka klabu moja kubwa Norway ambapo yuko kwenye mvutano na uongozi akishinikiza kuvunja mkataba wake
Suala lake linataka kufanana na lile la Coastal Union kuhusu Lameck Lawi ambaye tayari yuko Ubelgiji kukamilisha taratibu za kujiunga na KRC Genk
Coastal Union walipata ofa hiyo wakiwa tayari wako kwenye mchakato wa kumuuza Lawi Simba na ghafla kuamua kusitisha mazungumzo na Simba pamoja na kurejesha fedha walizokuwa tayari wamepokea kutoka kwa Simba
Post a Comment