Kibu apata timu Norway, ataka kurudisha mpunga wa Simba

Kibu apata timu Norway, ataka kurudisha mpunga wa Simba

Usikose kuitazama mechi ya YANGA vs TS GALAXY FC michuano ya Mpumalanga cup Live hapa bure

Ni kesho saa 10: 0 jioni usikose kuitazama mechi hii LIVE bure kupitia simu yako download app yetu mapema ili uweze kuitazama mechi hii kudownload app yetu bonyeza 👉🏻HAPA

Kibu apata timu Norway, ataka kurudisha mpunga wa Simba

Tetesi zinaeleza kuwa, kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Simba, Kibu Denis amaepata ofa nono kutoka klabu ya Tromsgodset ya Ligi Kuu nchini Norway ambako ametimkia kwa ajili ya kukamilisha dili hilo.

Kibu ambaye ameongezewa mkataba na Simba hivi karibuni mpaka mwaka 2026, anafikiria kurejesha pesa za usajili za Simba kama Release Clause ili awe huru kujiunga na timu hiyo na tayari amewasiliana na viongozi wa Simba ila wamemgomea.

Kwa upande wake, Meneja wa mshambuliaji wa Simba Sc, Kibu Dennis, Carlos amefichua kuwa mchezaji huyo yupo Ulaya licha ya kuwa amelipwa stahiki zake zote na haidai Simba Sc chochote huku akibainisha kuwa yeye binafsi ila suala hilo mwenye mamlaka ya kuliongelea ni Simba.

Hata hivyo Carlos hajaweka bayana kuwa Kibu yupo nchi gani huko Ulaya lakini maelezo yake yanaashiria nyota huyo yupo Ulaya kwa ajili ya majaribio.

"Simba ndiyo wanaweza kusema kama amekwenda majaribio au amepata timu au amewaaga au kuna jambo lolote, lakini mimi siwezi kumzungumzia kwa sababu hilo liko chini yao," amesema Carlos.

Aidha, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Sc, Ahmed Ally amesema hana taarifa za nyota huyo kuwa Ulaya na kwamba yeye anachojua Kibu yupo Kigoma huku akiongeza kuwa mwenye nafasi nzuri ya kuzungumzia sababu za Kibu kutokwepo kambini ni mchezaji mwenyewe.

"Mara ya mwisho taarifa niliyopewa ni kwamba Kibu alielekezwa alete passport yake ili akatiwe VISA aungane na wenzake, lakini mpaka sasa hajaleta. Sisi kama taasisi tumefanya kila kinachowezekana lakini mchezaji ndiye hajatimiza wajibu wake.

"Tunazo kanuni za miongozo ya klabu ambapo akiitwa akazungumza basi kila kitu kitawekwa wazi. Sisi hatujui kama amepata timu wala hatuna wasiwasi kwa sababu tuna mkataba nae mpya kabisa na taratibu anazijua kwamba yeye klabu inatakiwa ije tuzungumze," amesema Ahmed.

KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA


PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE  HAPA

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post