Khomein ni suala la muda Yanga
Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga wamefanya mazungumzo na Singida Fountain Gate kwa ajili ya kumsajili mlinda lango Khomeini Abubakari ambaye amebakisha mkataba wa mwaka mmoja klabuni hapo
Khomein alijiunga na Singida Fountain Gate akitokea Geita Gold ambapo msimu wa 2022/23 alikuwa kwenye tatu bora ya wanaowania tuzo ya kipa bora
Yanga tayari imeachana na mlinda lango Metacha Mnata baada ya mkataba wake wa mwaka mmoja na nusu kumalizika
Jana Yanga pia ilitangaza kumuongezea mkataba wa miaka miwili mlinda lango namba moja Djigui Diarra huku pia kipa namba mbili Aboutwalib Mshery nae akitarajiwa kusaini mkataba mpya
Ni wazi Khomein ndiye atakayerithi mikoba iliyoachwa na Metacha
Post a Comment