Meneja wa Kitengo cha habari na Mawasilino wa Yanga Ali Kamwe amewaaga mashabiki na wanachama wa timu hiyo baada ya mkataba wake kumalizika
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, jana usiku Kamwe aiiweka chapisho la kuwaaga Wananchi baada ya utumishi adhimu wa miaka miwili
"A Good dancer must know when to Leave a Stage. Mtumbuizaji mzuri anatakiwa kujua ni wakati gani wa kuondoka jukwaani"
"Maneno ya hekima kutoka katika kinywa cha Patrick Loch Otieno Lumumba; Na ni Hekima hii, inanituma mbele yenu Wananchi, Mashabiki na Wanachama wa Klabu yetu pendwa, kuwaambia kuwa, Ni wakati sasa wa kijana wenu kuondoka Jukwaani"
"Nimesimama Miaka miwili juu ya hili Jukwaa, Tumeimba, Tumecheza, Tumefurahi na Alhamdulillah Tumeshinda pamoja kila pambano Lililokuja mbele yetu"
"Muda wangu umemalizika na Asanteni sana. Tutaonana tena Wakati mwingine nikiwa na kitu kizuri cha kuwaonyesha Juu ya Jukwaa," aliandika Kamwe
Kamwe alitambulishwa Yanga mwaka 2022 akichukua nafasi ya Hassan Bumbuli ambaye mkataba wake ulimalizika
Hata hivyo bado Wananchi wanamuhitaji Kamwe na pengine huenda wakaendelea kuwa nae lakini akiwa na majukumu mapya
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Post a Comment