Wakati Simba ikiwa katika wiki ya pili ya pre-season inayoendela nchini Misri, kiungo mshambuliaji Kibu Denis sio miongoni mwa wachezaji wanaoshiriki pre-season hiyo
Kumekuwa na maswali mengi miongoni mwa mashabiki wa Simba wakitaka kufahamu kulikoni Kibu hayuko Misri?
Uongozi wa Simba haujatoa taarifa rasmi lakini inaelezwa winga huyo ana ruhusa
"Kibu alimaliza msimu uliopita akiwa majeruhi hivyo bado anaendelea na taratibu za kitabibu, nafikiri ataungana na timu pale atakapokuwa sawa," alisema mtoa taarifa
Kibu na Aishi Manula ndio wachezaji pekee ambao hawako kambini Misri suala la Manula nalo likifanana na Kibu kwani pia alipata majeraha wakati akiitumikia timu ya Taifa mwishoni mwa msimu uliopita
Aidha kuna taarifa kuwa Azam Fc walimtaka Manula, Simba ikaonyesha utayari wa kumruhusu lakini ikitaka kumtumia kama sehemu ya makubaliano ya kumsajili Feisal Salum 'Fei Toto' dili ambalo Azam Fc waligomea
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Post a Comment