Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema mshambuliaji Prince Dube bado hana utimamu wa kiuchezaji kwa asilimia 100 kutokana na kutocheza soka kwa muda mrefu
Akizungumza jana kuelekea katika mchezo wa leo wa Kombe la Mpumalanga dhidi ya TS Galaxy, Gamondi, alisema Dube hayupo kwenye kiwango chake ndiyo maana ubora wake haukuonekana katika mechi dhidi ya Augsburg ya Ujerumani, ambao walichapwa mabao 2-1
"Nafikiri wachezaji walicheza vizuri mechi iliyopita, lakini baadhi hawakufanya vizuri kwa sababu hawajacheza muda mrefu, mfano Dube, hakuwa uwanjani kwa zaidi ya miezi sita, Baleke alikuwa na afadhali kidogo, lakini wengine wanaonekana wako fiti, ila bado baadhi wanatakiwa wazoeane na wenzao, kujua wenzake wanapasiwa vipi mpira, na yeye mwenyewe mchezaji anatakiwa awe wapi ili apokee pasi kutoka kwa wenzake"
"Kiujumla kuna baadhi ya wachezaji wanatakiwa wazoeane na wenzao ili kujua wachezeje, ila kwa ujumla kila kitu kinakwenda sawa," alisema Gamondi
Mara ya mwisho Dube kuonekana uwanjani akicheza mechi ya ushindani ilikuwa ni Februari 9, mwaka huu, wakati timu yake ya Azam ikicheza dhidi ya Simba katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, timu hizo zikitoka sare ya bao 1-1
Mzimbabwe huyo akipachika bao dakika 14, kabla ya kusawazishwa na Mzambia, Clatous Chama dakika ya 90, na wote hao wamesajiliwa na Yanga kuelekea msimu ujao wa mashindano
Akizungumza mechi ya leo, Gamondi alisema atahakikisha kila mchezaji anapata fursa ya kuonyesha uwezo wake kwa sababu hakuna idadi maalum ya kuingiza wachezaji wa akiba
"Nitampa nafasi kila mchezaji kucheza angalau kwa dakika 15 ili kuonyesha uwezo walionao na kuwafanya wawe na utimamu wa mwili, tunakwenda hivyo hivyo taratibu, kidogo kidogo lakini kwa uhakika," alisema Gamondi
Baada ya mechi hiyo, Yanga itakamilisha mechi zake Jumapili, ambapo inatarajiwa kucheza mchezo wa Kombe la Toyota, dhidi ya Kaizer Chief ya nchini humo itakayopigwa Uwanja wa Bloemfontein
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Post a Comment