Chama apagawa na 'Welcome' ya Wananchi
Kiungo mshambuliaji wa Yanga Clatous Chama amewashukuru mashabiki na wanachama wa Yanga kwa ukaribisho wa aina yake
Jana Yanga ilimtambulisha Chama kwa utambulisho rasmi baada ya hapo awali kumtambulisha kupitia picha za kusaini mkataba
Chama amesema amefurahia na vile Wananchi walivyompokea na kuwaahidi kuwafanyia mambo makubwa uwanjani
"Nafurahi kujiunga na timu hii kubwa zaidi Tanzania. Nawashukuru Wananchi kwa mapokezi yao kwa kweli nimepokelewa vizuri"
"Sitazungumza mengi kwa sasa lakini nawaahidi, watafurahi uwanjani," alisema Chama
Baada ya usajili wake kutangazwa wiki iliyopita, Wananchi wakiongozwa Msemaji wa klabu Ali Kamwe waliandamana mitaani kufurahia usajili wake
Kama haitoshi likafanyika tukio maalum la kula keki Makao Makuu ya Yanga, Jangwani ambapo keki 17 zililiwa na Wananchi ikiwa ishara ya kumkaribisha Chama nayependelea kuvaa jezi namba 17
Chama tayari ameungana na kikosi cha Yanga kilichoanza maandalizi ya pre-season. Yanga inatarajiwa kuelekea Afrika Kusini wiki ijayo kwa ajili ya maandalizi ya Toyota Cup ambapo Julai 28 watachuana na Kaizer Chiefs
Post a Comment