Aziz Ki amkaribisha Dube Yanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Aziz Ki amkaribisha Dube Yanga

Aziz Ki amkaribisha Dube Yanga


Usikose kutazama live mechi za EURO 2024 bure kwenye simu yako download app yetu kutazama pia chanel za Azam tv zote bure kudownload app yetu bonyeza 👉🏻 HAPA


 Kama alivyofanya kwa Clatous Chama, kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki amemkaribisha Prince Dube 'Mwana Mfalme' ambaye Yanga ilithibitisha kukamilisha usajili wake usiku wa kuamkia Jumapili

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Aziz Ki aliweka chapisho la kumkaribisha Dube huku akimtaja kama mfungaji bora wa Ligi Kuu 2024/25

Ni wazi Aziz Ki alikuwa akisubiri kwa hamu utambulisho wa mshambuliaji huyo wa zamani wa Azam Fc, akionekana kumkubali

Aziz Ki alikuwa mchezaji wa kwanza kufichua usajili wa Dube katika moja ya mahojiano yake katika mitandao ya kijamii

Aziz Ki aliweka bayana kuwa msimu ujao hana mpango na tuzo ya mfungaji bora kwani atahakikisha tuzo hiyo inabebwa na washambuliaji wa Yanga zaidi akimtaja Dube

NMsimu ujao Dube na washambuliaji wenzake katika kikosi cha Yanga washindwe wenyewe tu katika kuzifumania nyavu kwani kikosi kimesheheni wapishi wa kuwatengenezea nafasi

Chama, Aziz Ki, Pacome Zouzoua, Maxi Nzengeli wote watakuwa kazi moja tu, kuwatengeneza nafasi lakini pia hawataacha kufunga kama walivyofanya msimu uliopita

KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA


PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE  HAPA



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz