Ally kamwe atamba kuelekea mechi ya kesho dhidi ya Augsburg
Ni kesho Yanga vs Augsburg michuano ya mpumalanga iliyoandaliwa afrika kusini usikose kuitazama mechi hii live bure kupitia simu yako download app yetu kutazama mechi hii live bure pia ndani ya app yetu zipo chanel za azam tv pia utaweza kutazama muvi zilizo tafsiriwa kudownload app yetu bonyeza 👉🏻HAPA
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema August 08 wataitumia 'kushona' midomo ya wale wanaoamini kuna timu zimekaribia daraja la Yanga baada ya usajili wa dirisha hili
August 08 Yanga itachuana na Simba katika mchezo wa nusu fainali Ngao ya Jamii utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Akizungumza muda mfupi baada ya kutua Afrika Kusini ambako Yanga itashiriki michuano maalum ya Mpumalanga, Kamwe amesema baada ya maandalizi na mechi watakazocheza katika pre-season hapo Afrika Kusini, anaamini watarejea nchini wakiwa tayari kuwapa furaha mashabiki wao
"August 08 ni siku ya kuwashona midomo watu! Unajua kuna watu wanaamini timu zao zimekaribia daraja la Yanga hivyo siku hiyo tutakwenda kuwaonyesha Yanga iko katika daraja lake tofauti," alitamba Kamwe
Katika hatua nyingine, Kamwe amesema wanatarajia mchezo dhidi ya Augusburg utakaopigwa kesho huko Mpumalanga utakuwa mgumu licha ya kuwa ni mechi ya pre-season
Yanga iltua Afrika Kusini jana usiku na kupokelewa mashabiki wengi katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo
Yanga na Augusburg zilikutana uwanja wa ndege lakini kilichowashangaza Wajerumani hao ni msisimko mkubwa wa mashabiki kuonakena upande wa Yanga kuliko wao licha ya kuwa ni timu inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani
Kamwe amesema amekuwa na mawasiliano na Afisa Habari wa Augusburg ambaye amekiri kushangazwa na hamasa kubwa ya mashabiki wa Yanga ambao kama kawaida yao wamevamia kurasa za mitandao ya kijamii za klabu hiyo 'kuwapiga mkwara'
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Post a Comment