Kocha na daktari wa viungo wa Yanga, Mtunisia, Youssef Ammar aliyekuwa akielezwa kuwa ni kipenzi cha wachezaji wengi amesepa kimyakimya.
Sababu kubwa ikitajwa ni mkataba wake umemalizika na uongozi umeshindwa kufikia makubaliano ya kumuongezea.
Ammar aliachwa Yanga na kocha aliyeondoka, Nasreddine Nabi. Moja ya sifa za hivi karibuni kwa Kocha huyo ni kumrejesha haraka kwenye ubora wake, Khalid Aucho aliyekuwa na majeraha ambayo wengi walidhani angekosa mechi zaidi ya nusu msimu.
Lakini inaelezwa kuwa FAR Rabat ya Morocco ilimrejesha nchini, Bernard Morrison aje akatibiwe kwaajili yake kwani Nabi anamuelewa zaidi.
"Yalikuwa ni maamuzi ya upande mmoja, maamuzi hayakuwa kwa asilimia 100% kutoka Yanga bali uongozi wa Yanga umelazimishwa kufanya haya maamuzi na yamefanywa na mkuu wa benchi la ufundi Kocha Gamondi."- Youssef Ammar, Daktari.
BONYEZA HAPA KUANGALIA VIDEO ZA XX ( WAKUBWA ) UJIFUNZE MAUTUNDU
Post a Comment