Baada ya kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu, kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki amesema hatarajii kushinda tuzo hiyo msimu ujao kwani kazi yake itakuwa kuhakikisha anawatengenezea nafasi washambuliaji waliosajiliwa
Aidha, kauli hiyo ya Ki ambayo aliitoa wakati akifanya mahojiano ya 'live' katika mtandao wa Instagram, imewapa uhakika Wananchi kuwa ataendelea kuitumikia Yanga msimu ujao
"Kwa nini unataka mimi niwe mfungaji bora msimu ujao? Mimi ahadi yangu, nina matumaini straika wa Yanga atakuwa mfungaji bora msimu ujao Mungu akipenda, lakini sio Aziz, sahau kuhusu Aziz, mimi nitatoa asisti na siyo kuwa mfungaji bora"
"Nafahamu Dube (Prince) anakuja na Guede(Joseph) yupo mimi ni kiungo, nitafanya kila liwezekanalo kuhakikisha wanakuwa wafungaji bora. Mimi ni kiungo kwa nini niwanie ufungaji bora, kwa nini ununue straika halafu utake kiungo awe mfungaji bora?” alihoji Aziz Ki na kuongeza
Kauli ya Aziz Ki pia inathibitisha kuwa pengine ni suala la muda tu, Yanga itamtambulisha mshambuliaji wa zamani wa Azam Fc Prince Dube kuwa ni Mwananchi
Dube aliikacha Azam Fc katikati ya msimu uliopita akihitaji changamoto mpya
BONYEZA HAPA KUTAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA UJIFUNZE MAUTUNDU YA CHUMBANI
Post a Comment