Klabu ya Yanga leo Jumapili inafanya Mkutano Mkuu wa Mwaka huku ikielezwa kutakuwa na sapraizi ya aina yake kutoka kwa viongozi kabla na baada ya mkutano huo unaofanyikia kwenye Ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam kuanza saa 3 asubuhi.
Mkutano huo utakaokuwa na ajenda 10 ni wa pili tangu viongozi wa sasa walipochaguliwa Julai mwaka juzi na Injinia Hersi Said na Arafat Haji pamoja na wajumbe wengine walichaguliwa na Juni mwaka jana walifanya mkutano uliweka bayana mapato na matumizi ya klabu hiyo.
Kwa mujibu wa Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said mkutano huo utakuwa na ajenda 10 huku akiwataka wajumbe wote wa mkutano mkuu kuhudhuria na mkutano huo ni kwa mujibu wa ibara ya 20 ya Katiba ya Yanga ya mwaka 2021, hata hivyo, Mwanaspoti imepenyezewa kutakuwa pia na sapraizi ya aina yake leo ukumbini.
Mikutano miwili tofauti Yanga iliwasapraizi wanachama kwa kuwatambulisha wachezaji wapya ukumbini akiwamo Juma Balinya na Gael Bigirimana na leo inaelezwa kuna nyota maarufu aliyewahi kuwika Simba huenda akatambulishwa mbali na ufafanuzi ya dili za Kocha Miguel Gamondi na Stephane Aziz KI.
Taarifa za uwepo kwa straika wa zamani wa Simba aliyekuwa akikipiga Libya, Jean Baleke na kukamilika kwa dili la baadhi ya wachezaji inayowawinda kwa msimu ujao ni mambo yaliyoongeza mzuka wa mkutano huo.
Hata hivyo, Hersi alitaja ajenda za mkutano huo wa kawaida ni; kufungua mkutano, uhakiki wa wajumbe watakaoudhuria mkutano, kuthibitisha ajenda, kuthibitisha kumbukumbu za mkutano uliopita, yatokanayo na mkutano uliopita.
Post a Comment