Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba wameridhia uamuzi wa Rais wa heshima wa klabu hiyo, Mohammed Dewj ‘MO’ akiwataka waachie ngazi.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kimeliambia Mwanaspoti viongozi wote wa bodi ya Simba wametii wito wa kiongozi wao ambaye ndiye aliyewateua.
“Hadi sasa wajumbe wote wamejiuzulu kama mambo yataenda sawa kesho au keshokutwa Barbara Gonzalez atatangazwa kuwa Mwenyekiti huku CEO anatafutwa,” kimesema chanzo hicho na kuongeza;
“Simu hizo amewapigia wajumbe wa upande wake pekee kwani ndio ana uwezo wa kufanya uamuzi huku kwa upande wa klabu viongozi waliopitishwa na wanachama kwenye mkutano mkuu wanaendelea na majukumu yao kama kawaida,” kimesema chanzo hicho.
Wajumbe hao wa bodi waliokuwa chini ya Mwenyekiti Salum Abdallah 'Try Again' ni Dk Raphael Chageni, Hamza Johari, Zulfikar Chandoo na Rashid Shangazi.
Post a Comment