Tetesi za usajili ligi kuu tz bara leo Jumapili

Bryan Mandela Onyango

Kivumbi cha mataifa ya africa kuwania kufuzu kombe la dunia kinaendelea leo usikose kuzitazama mechi hizi live buree kwenye simu yako bonyeza hapa kudownload app inayorusha mechi hizi live buree kabisa kumbuka kuna mechi ya Zambia vs Tanzania kesho kutwa usikose bofya sasa kudownlod app hii mapema ili kuepuka usumbufu siku ya mechi pia app hii ina muvi zilizotafsiriwa kwa kiswahili pamoja na chanel za azam tv na dstv

Simba imefanya mazungumzo ya kumpata beki wa KVZ ya Zanzibar, Salum Athuman ‘Stopper’ ambaye amekuwa na kiwango bora.

Zao hilo la timu ya vijana ya Simba, aliyewahi kucheza pia Fountain Gate, JKT TZ na Mbeya Kwanza,  amekuwa katika kiwango bora na ikielezwa Msimbazi walimfuatilia kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi na Muungano iliyofanyika mwaka huu Zanzibar.

Msimbazi wamtaka Onyango

Simba inatumia inajipanga kumpata beki wa kati wa Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini Mkenya, Brian Mandela Onyango.

Onyango mwenye miaka 29 ameshindwa kupata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza kwenye timu hiyo jambo ambalo mabosi wa Simba wanalitumia kama fursa ya kumpata, huku akiwahi kupita timu mbalimbali zikiwemo Tusker FC na Maritzburg United FC.

Karihe na Mashujaa FC

Mashujaa imeanza mazungumzo na aliyekuwa mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Seif Karihe ili kuwaongezea nguvu msimu ujao. Nyota huyo aliyefunga mabao saba Ligi Kuu msimu uliopita akiwa na Mtibwa iliyoshuka daraja, anatafuta timu ya kujiunga nayo msimu ujao na Mashujaa inatajwa kumhitaji ili kwenda kuziba nafasi ya Adam Adam aliyetua Azam FC.

Bangala na Simba

Viongozi wa Simba wamewasiliana na wakala wa kiungo, Yannick Bangala anayeichezea Azam FC ili kuangalia namna ya kumpata nyota huyo raia wa Congo. Taarifa zinaeleza, baada ya kuzungumza na wakala wa Bangala itawafuata Azam kumalizana nao ili nyota huyo alaiyewahi  kucheza Yanga, AS Vita ya Congo na FAR Rabat ya Morocco atue Msimbazi.

Tariq anukia Pamba Jiji

PAMBA Jiji imeanza kusuka mapema kikosi ikitajwa kumsaka kiungo wa Tanzania Prisons, Tariq Simba. Simba aliyewahi kukipiga Polisi TZ na Geita Gold amebakisha mkataba wa miezi sita Prisons na baadhi ya viongozi wa Pamba wameanza mawasiliano naye na wapo tayari kumchukua japo waajiri wake wa sasa nao inadaiwa bado wanamhitaji.

Makata aigeukia FGA

FGA Talents inadaiwa imeanza mazunguzo na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Pamba Jiji, Mbwana Makata ili ainone timu hiyo msimu ujao. Makata aliipandisha Pamba hadi Ligi Kuu msimu huu baada ya kusota kwa miaka 23, ameachana na kikosi hicho cha jijini Mwanza baada ya mkataba wake kumalizika, huku FGA ikimtaka baada ya kuzipandisha daraja pia Polisi TZ na nyingine.

Farid kwa Azam, KenGold

AZAM FC imedaiwa kuanza mazungumzo ya kumrudisha winga wa zamani wa timu hiyo, Farid Mussa aliyemaliza mkataba na Yanga. Farid amewahi kuichezea Azam kati ya 2013- 2016 kisha kwenda Hispania kabla ya kutua Yanga 2020 na amekuwa hapati namba kikosi cha kwanza. Anatajwa kuwindwa pia na KenGold na Singida Black Stars.

BONYEZA HAPA KUANGALIA VIDEO ZA WAKUBWA UJIFUNZE MAUTUNDU

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post