Kiungo Zawadi Mauya ataendelea kuwatumikia Wananchi baada ya makubaliano ya kuongeza mkataba wa mwaka mmoja kufikiwa
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga imebainisha kuwa Kocha Miguel Gamondi amependekeza Mauya aongezwe mkataba baada ya mkataba wake wa awali kumalizika
Ni baada ya Muargentina huyo kujiridhisha hakuna wachezaji wengi wa ndani wanaocheza nafasi ya Mauya ambao ni bora kuliko yeye
Yanga huenda isiwe na ingizo jipya kwenye safu ya kiungo cha ukabaji ambapo Mauya, Jonas Mkude, Khalid Aucho, Mudathir Yahya na Salum Abubakar 'Sure Boy' wataendelea kuhudumu katika eneo hilo
Aidha, imeelezwa Gamondi amependekeza usajili wa wachezaji wanne kuongeza nguvu katika maeneo ya safu ya ulinzi (pembeni), winga na eneo la ushambuliaji
BONYEZA HAPA KUANGALIA VIDEO ZA WAKUBWA UJIFUNZE MAUTUNDU YA KITANDANI
Post a Comment