Straika la mabao Kotoko laingia rada za Simba

Straika la mabao Kotoko laingia rada za Simba

Leo kivumbi cha mataifa ya africa kufuzu kombe la dunia kinaendelea ambapo kenya, uganda, burundi zitashuka uwanjani na nyingine nyingi usikose kuzitazama mechi hizi zote live bure kwenye simu yako bonyeza hapa kudownload app inayorusha mechi hizi live bure kabisa pia kwenye app hii kuna muvi zilizotafsiriwa kwa kiswahili pamoja na chanel za azam tv na dstv bofya sasa kuidownload uweze kufurahia chanel mbali mbali

Simba wako siriazi na mambo yanakwenda kimyakimya. Mwanaspoti linajua mpaka jana jioni kwa uchache ilishamalizana na majembe mawili.

Lameck Lawi (Coastal Union) huyu ni beki. Serge Pokou (Asec) ni kiungo. Lakini hata Yusuph Kagoma (Singida FG) kila kitu kimeshakamilika kwa asilimia kubwa. Ishu ya kocha wako kwenye hatua za mwisho kumalizana na Steve Komphela kutoka Afrika Kusini.

Sasa imefikia pazuri kumsainisha mkataba wa miaka miwili straika wa Uganda, Steven Dese Mukwala (24) na Elie Mpanzu wa AS Vita.

Mukwala anakiwasha kwenye klabu ya Asante Kotoko ya Ghana. Wekundu wa Msimbazi hao wamepania kurejesha ufalme wao uliofifia kwa misimu mitatu nyuma ambapo wameamua kuvunja benki ili kushusha wachezaji wa maana.

Mukwala leo Ijumaa atakuwa kwenye Uwanja wa Mandela nchini Uganda akiiongoza timu yake ya taifa, kuivaa Botswana katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia.

Mukwala ni mfungaji bora namba mbili katika msimu uliomalizika wa ligi ya Ghana akifunga mabao 14 nyuma ya kinara Stephen Amankonah wa Berekum Chelsea aliyecheka na nyavu mara 16.

Straika huyo anayesifika kwa kasi, mashuti na umahiri wa kufunga amemaliza mkataba na Kotoko lakini wakali hao wa Ghana wameonyesha nia ya kumuongezea mkataba mpya ila Mukwala amegoma kusaini huku akiwaeleza anaondoka kwenda kutafuta changamoto mpya.


Mwanaspoti limegundua Simba ndiyo imempa kiburi Mukwala kutoongeza mkataba mpya kwa kumuahidi kumsaini na kumpa bonasi kubwa jambo lililomvutia haswa akiangalia hamasa iliyopo kwenye ligi hiyo kwasasa.

Mwanaspoti linajua Simba imewasiliana na Mukwala na pande hizo mbili zimekubaliana kukutana baada ya mechi za timu za taifa kwa mazungumzo ya mwisho ya dili hilo.

“Kama kila kitu kitaenda tulivyopanga basi atasaini mkataba wa miaka miwili,” alidokeza mmoja ya viongozi wa juu wa Simba ambayo imeunda kamati mpya ya usajili yenye sura zenye uzoefu kama Cresentius Magori, Mulamu Nghambi na Kassim Dewji.

Kwa kauli hiyo, Mukwala huenda akatua nchini baada ya Juni 10, kwani siku hiyo timu yake ya Uganda The Cranes itakuwa na mechi dhidi ya Algeria itakayochezwa kwenye uwanja wa Mandela.

Mukwala aliyeibuka mchezaji bora wa ligi ya Ghana kwa mwezi Desemba mwaka jana alijiunga na Kotoko Agosti 2022 akitokea URA ya Uganda na katika msimu wake wa kwanza alifunga mabao 11 na kutoa asisti tano.

Akiwa URA Mukwala alicheza kwa misimu mitatu kuanzia mwaka 2020 ambapo msimu wa kwanza 2019/20 aliibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Uganda akifunga mabao, msimu uliofuata wa 2020/21 akafunga mabao 14 na msimu wake wa mwisho yaani 2021/22 akacheka na nyavu mara 13 hivyo ana wastani wa kufunga mabao zaidi ya 10 kwa kila msimu.

Straika huyo alianza soka la ushindani mwaka 2017 alipojiunga na Vipers akitokea Masaza FC kisha Maroons kabla ya kurejea Vipers na baadaye URA, pia amepita kwenye timu zote za taifa za Uganda kwa vijana.

Mukwala anaungana na kiungo wa Asec Mimosac ya Ivory Coast, Sergie Pokou na winga wa AS Vita ya DRC, Elie Mpanzu katika meza ya uamuzi ya Simba ambapo wote huenda kwa msimu ujao wakavaa uzi mwekundu na mweupe kama watakubaliana na mabosi wa Msimbazi.

KUHUSU KINZUMBI, MPANZU

Mwanaspoti linajua Simba imebadili gia angani baada ya kushindwa gharama za kumpata kiraka wa TP Mazembe, Philip Kinzumbi. Sasa imemgeukia Elie Mpanzu wa AS Vita.

Habari za uhakika ambazo Mwanaspoti inazo ni kwamba licha ya kuwa ni mchezaji mzuri ila uongozi wa Mazembe umeweka dau kubwa ambalo kwa upande wao sio rahisi kulitoa kwa sasa.

Habari zinasema Simba itampa Sh260 milioni kama gharama za mkataba wa misimu miwili lakini mshahara wake utakuwa mkubwa.

“Ukimtazama Kinzumbi na Mpanzu utaona ni kama wako daraja moja la ubora, msimu huu Mpanzu amekuwa na kiwango bora zaidi akiwa na klabu yake, tukifanikiwa kumalizana na klabu yake tutakuwa tumepata mtu sahihi kwa klabu yetu,” alidokeza mmoja wa viongozi wa Simba.

Wekundu hao kwanza walitua kwa winga wa TP Mazembe, Kinzumbi anayejua kushambulia akichezea mguu wa kushoto lakini timu yake imehitaji gharama kubwa, hata hivyo wekundu hao wameshtukia dili kuwa ofa za kutoka klabu kubwa za Afrika Kaskazini, ndizo zilizochangia bei ya winga huyo kuwa za juu.

Baada ya ugumu huo, Simba imegeukia upande wa pili, kumpata kiungo mshambuliaji mwingine kutoka nchi hiyohiyo, Elie Mpanzu, anayoichezea AS Vita.

Mpanzu ndiye staa wa Vita Club inayopambana kujirudisha kwenye viwango vyake vya juu baada ya kupitia anguko kubwa la kiuchumi, staa huyo ndiye injini ya mabao akiwa amefunga mabao 16 msimu huu uliomalizika.

Mpanzu amebakiza mkataba wa miaka miwili na Vita Club ingawa kocha wa timu hiyo bado anamuhitaji lakini Simba inaweza kumpata kama itaweka dau zuri mezani.

Ukiachana na mastaa hao wawili, Mwanaspoti linajua tayari Simba imeshamalizana na kiungo wa Asec Memosas, Serge Pokou na atasaini wiki hii kuwatumikia wababe hao wa Msimbazi.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post