Simba yashusha kiungo Mcongo
Klabu ya Simba inatajwa kukamilisha usajili wa kiungo kutoka Jamhuri ya Congo Debora Mavambo Fernandesn (mwenye jezi nyeupe pichani juu) aliyekuwa aakiitumikia Mutondo Stars ya Ligi Kuu Zambia (MTN)
Kiungo huyo wa kati mzaliwa wa Angola mwenye umri wa miaka 24 tayari yuko nchini na huenda akawa miongoni mwa wachezaji watakaotambulishwa na Simba siku chache zijazo
Debora ameitumikia Mutondo FC msimu mmoja akijiunga akitokea klabu ya Academica Petroleos do Lobito ya Angola mwaka 2023
Kiungo huyo anamudu kucheza eneo la kiungo mkabaji lakini pia mara chache ametumika katika safu ya ulinzi
Ujio wa Debora huenda ukashuhudia Simba ikiachana na Sadio Kanoute au Babacar Sarr
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amesema uongozi uko kwenye majadiliano ya kusitisha mikataba ya baadhi ya wachezaji
Taarifa za wachezaji hao kupewa 'Thank You' zitatolewa baada ya michakato hiyo kumalizika
Post a Comment