Simba yashtuka, kuja kivingine

Simba yashtuka, kuja kivingine

Ni kesho ZAMBIA vs TANZANIA mechi ya kuwania kufuzu kombe la dunia usikose kuitazama mechi hii live bure kwenye simu yako bonyeza hapa kudownload app itakayoonesha mechi hii live bure kabisa pia ukiwa na app hii utaweza kutazama muvi zilizotafsiriwa kwa kiswahili pamoja na chanel za Azam tv na Dstv bure bofya sasa kuidownload

Katika kuhakikisha Simba SC inarudi kwa kishindo, klabu hiyo imesema imejipanga kufanya usajili kwa umakini mkubwa ili kutorudia makosa ya nyuma na uongopzi wa Msimbazi umetangaza kuja na sera ya usajili.

Kwa misimu mitatu mfululizo Simba imeshindwa kuwa na maajabu katika Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho, huku ikikwamia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa mfululizo na sasa kumekuwa na sintofahamu katikam uongozi, lakiini imebainika Mnyama ameshtuka na anajipanga kimyakimya.

Sera hiyo ambayo Simba imepanga kuja nayo, imesema itaifanya kusajili wachezaji wenye sifa za kuitumikia timu hiyo na si kujaza wachezaji wasiokuwa na tija ambao mwisho wanapata shida katika kuvunja mikataba yao.

Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Simba ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, Dk. Seif Muba, amesema: Tumeiambia ofisi ya CEO ya Simba itengeneze sera ya usajili ambayo itatumika kusajili wachezaji na kuwaondoa, sera hii itakuwa maalum ambayo tutaitumia wote. Hata ikitokea mimi na wenzangu tukatoka ndani ya uongozi hiyo sera ibaki palepale.â€

Katika kukazia hilo, Issa Masoud ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi wa Fedha Simba na Mjumbe wa Bodi wa klabu hiyo, amesema sio suala la usajili pekee, pia kamati yoyote hata ile ya usajili ambayo inatajwa kuanzishwa, lazima ifuate utaratibu uliopo.

“Jambo lolote linalofanyika ndani ya Simba ambalo haliendani na katiba yetu hilo haliruhusiwi, tumekuwa tukisikia kwamba kuna Kamati ya Usajili imeanzishwa, huo sio utaratibu.


“Kamati yoyote ndani ya Simba inaundwa na Bodi, nje ya Bodi hiyo kamati hatuitambui. Na tumesema sasa hivi hata usajili utakaofanyika nje ya bodi, huo hatuutambui kwa sababu hatutaki kukiuka utaratibu.

“Kama kuna mchezaji huko atasajiliwa au kocha ataletwa na hajapita katika utaratibu, basi ataenda timu nyingine, hatakuwa ndani ya Simba, hata kama akisajiliwa Cristiano Ronaldo bila ya kupitia kwenye utaratibu wa Bodi atatafuta sehemu ya kuchezea.

“Tumekuwa tukisajili wachezaji wengine wakiwa hawana viwango tunavyovitaka, mwisho wa siku haohao waliomsajili wanakuja kusema mwacheni, akiachwa mchezaji anaacha madeni, klabu imekuwa ikiongezewa madeni yasiyokuwa na vichwa wala miguu. Mwisho wa siku tunatakiwa kufuata utaratibu hata ikitokea kuna deni tunapaswa kulikubali kwani tuliridhia.

BONYEZA HAPA KUANGALIA VIDEO ZA WAKUBWA ILI UJIFUNZE MAUTUNDU

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post