Benchi la ufundi la Simba limebainisha kuwa usajili ni muhimu kufanyika kwa ajili ya mabresho ya timu hiyo kwa msimu wa 2024/25 ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Ipo wazi kuwa kuna balaa zito linakuja ndani ya Simba kwenye upande wa usajili kwa kuwa kuna wachezaji ambao wataondoka na wapo ambao wataongezewa kandarasi mpya.
Miongoni mwa wachezaji ambao taarifa zinaeleza kuwa wamesaini madili mapya ni Mzamiru Yassin kiungo wa kazi na Israel Mwenda beki wa kupanda na kushuka.
Taarifa kutoka kwenye benchi la ufundi lililo chini ya Juma Mgunda zimeeleza kuwa mpango mkubwa ni kuwapa kazi kubwa wachezaji wapya na wale ambao watabaki ndani ya kikosi ili kufanya vizuri kwenye mechi za ushindani.
“Kuna wachezaji wapya watakuja ndani ya Simba na wengine wataondoka kikubwa ni kuona kwamba kila mchezaji anakuwa bora na kutimiza majukumu yake kwa wakati kwa kuwa balaa zito linakuja msimu ujao.”
Kwa upande wa Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari Simba hivi karibuni aliweka wazi kuwa watafanya usajili mzuri na wapo wachezaji ambao wataondoka na wale watakaoongezewa mikataba.
BONYEZA HAPA KUANGALIA VIDEO ZA WAKUBWA UJIFUNZE MAUTUNDU YA KULOMBANA
Post a Comment