Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula amekutana na Kocha wa timu ya Vijana wa chini ya miaka 17, John Bocco.
Simba SC imemkabidhi Bocco jukumu la kukinoa kikosi cha vijana wa chini ya miaka 17 ambacho kimeonyesha mafanikio makubwa msimu huu.
Kajula alisema “tunatambua mchango mkubwa wa John Bocco ndani ya Simba kama nahodha wetu na sasa kocha kwenye timu zetu za vijana. Tunalenga mbali na kutumia wachezaji wetu wenye uzoefu na waliotumikia klabu yetu kwa mafanikio ni moja ya lengo letu katika kujenga timu imara za vijana.”
BONYEZA HAPA KUANGALIA VIDEO ZA WAKUBWA ILI UJIFUNZE MAUTUNDU
Post a Comment