Simba waamua hili kuhusu Kapombe
Ni yanga vs Safari champions usikose kuitazama mechi hii live bure kwenye simu yako pia mechi za EURO 2024 download app yetu inayorusha mechi hizi buree kabisa pia kwenye app yetu kuna muvi zilizo tafsiriwa kwa kiswahili pia kuna chanel za Azam tv na Dstv zote unazitazama buree download sasa App yetu kuenjoy bonyeza 👉🏻👉🏻HAPA
Simba imemuongezea mkataba wa mwaka mmoja beki wake wa kulia, Shomari Kapombe ambao ndani yake una kipengele cha akifanya vizuri ataongezewa mwingine.
Mwanaspoti limepata taarifa za ndani kuhusiana na Simba kumsainisha Kapombe, hivyo wakati wowote kuanzia sasa klabu hiyo itatangaza kuendelea naye msimu ujao wa 2024-2025.
"Tumemalizana na Kapombe, hivyo bado ni mchezaji halali wa Simba, tutaendelea kufaidi huduma yake na uzoefu wake kwani ni kati ya wachezaji wazawa ambao wana nidhamu ya kutunza vipaji na viwango vyao," kilisema chanzo kutoka ndani ya Simba.
Kabla ya Kapombe kuongezewa mkataba huo, alikuwa anahusishwa kujiunga na Singida Black Stars na Namungo ambapo mtoa taarifa wetu amebainisha kwamba: "Ni kweli Kapombe alipata ofa mbalimbali za timu za hapa ndani na nje.
"Mashabiki wa Simba waendelee kuamini viongozi wao wanasajili wachezaji wa maana, hivyo msimu ujao utakuwa wa burudani na kufurahia mafanikio."
Kapombe amekuwa ndani ya Simba tangu Julai 2017 alipojiunga na timu hiyo akitokea Azam FC ambapo amefanikiwa kuipa mataji manne mfululizo ya Ligi Kuu Bara 2017-2018, 2018-2019, 2019-2020 na 2020-2021.
Pia amekuwa sehemu ya mafanikio ya timu hiyo kucheza robo fainali tano katika misimu sita ya michuano ya kimataifa tangu 2018-2019 hadi 2023-2024.
Post a Comment