Simba kumshusha pacha wa Pacome na Aziz KI

 Serge Pokou.

Leo kuna mechi za kibabe Caf za kufuzu kombe la dunia bofya hapa kudownload app itakayoonesha mechi hizi zote live bure kwenye simu yako pia ndani ya app hii utaweza kutazama muvi zilizo tafsiriwa kwa kiswahili bure pamoja na chanel za azam tv na Dstv

habari za uhakika ni kwamba Simba wiki hii itamsainisha kiungo wa Asec Mimosas, Serge Pokou mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh200mil.

Hivi karibuni Mwanaspoti liliripoti kuwa Simba imefanya mazungumzo na kiungo huyo panga pangua wa Asec na wamekubaliana sehemu kubwa ya dili hilo, ili mwamba huyo aje akakipige kwenye kikosi hicho msimu ujao.

Tayari soko la wachezaji kutoka Asec limeshazoeleka hapa nchini, baada ya mastaa kama Stephane Aziz Ki, Pacome Zouazoua na Aubin Kramo kutoka huko kuja kukiwasha hapa nchini.

Muivory Coast, huyo mwenye mkataba wa mwaka mmoja na Asec, ana historia nzuri na Wekundu wa Msimbazi katika michuano ya kimataifa hatua ya makundi, baada ya kuwavurugia hesabu kwa kuwafunga bao la jioni (dakika 77) katika mchezo wa kwanza msimu huu, walipokutana kwenye Uwanja wa Mkapa uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, lakini pia alionyesha kiwango cha juu kwenye mchezo wa pili ugenini.

Habari za uhakika ambazo Mwanaspoti imezipata ni kwamba Simba wameshakamilisha asilimia kubwa ya dili la staa huyo na huenda muda wowote akasaini.

Awali klabu yake ilikomaa wakishinikiza kupata dau kubwa lakini badae wakakubaliana na Mnyama na watatumia gharama isiyozidi Sh200Mil.


Awali Pokou mwenye kasi na chenga za maudhi ambaye inaelezwa kuwa alishaomba kuondoka kwenye timu yake, alisema kila kitu kwake kipo sawa na anachosubiri kwa sasa ni tiketi tu kutoka Simba ili atue Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo ya mwisho.

“Nafikiri unakumbuka kuwa awali tulishafanya mazungumzo na Simba, sasa imebaki sehemu ndogo sana,nilipozungumza nao walianiambia nisubiri kidogo kwani watanipigia simu ili watume tiketi, huku wakisema kuwa mambo wanamalizia,” alisema Pokou.

Kirekodi msimu huu amewazidi viungo washambuliaji wa Simba ambao ni Clatous Chama na Saido Ntibazonkiza ambao wote ni wakongwe.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post