Simba Day kufanyika Agosti 3 - Video
Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu Simba, Ahmed Ally ametangaza rasmi kilele cha tamasha la Simba Day ambalo litafanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Agosti 3, 2024.
Kwa kawaida, tamasha la Simba Day hufanyika Agosti 8 kila mwaka lakini mwaka huu kutokana na kuwepo kwa michuano ya Ngao ya Jamii itakayoanza tarehe hiyo hiyo (Agosti 8), tamasha hilo wameamua kulirudisha nyuma ili kuendana na kalenda ya TFF kwa msimu ujao.
Kupitia taarifa rasmi ambayo ameitoa kwenye mitandao ya Kijamii ya Klabu ya Simba, Ahmed amesema;
“Leo tungependa kuwaambia wanasimba Duniani kote, tukio la Simba Day litajuwa Aug 03,2024. Ile wiki nzima itakuwa ya hekaheka. Tumeitangaza mapema ili watu wanaotoka mataifa mbalimbali waanze kuweka booking,” amesema Ahmed.
Post a Comment