Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limekiri kupokea barua ya kutaka kujiuzulu kwa nahodha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Mbwana Samatta ‘Samagol’, lakini imemkaushia kwamba hadi watakapofanya kikao cha pamoja ili kujadiliana naye.
Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao, amefafajua juu ya jambo hilo akisema kwamba hawapo tayari kumuona Samatta anajiuzulu kuitumikia timu ya taifa na wamepanga kukutana naye kwanza ili wazungumze.
“Huwezi kumuacha mchezaji mwenye CV kubwa kama yake, anajiuzulu kirahisi, sisi kama viongozi wa TFF, hatupo tayari kwa hilo, tutakaa chini kuzungumza naye,” alisema Kidao.
Post a Comment