Pacome aahidi balaa zito msimu ujao

Pacome aahidi balaa zito msimu ujao

Leo kuna mechi za kibabe Caf za kufuzu kombe la dunia bofya hapa kudownload app itakayoonesha mechi hizi zote live bure kwenye simu yako pia ndani ya app hii utaweza kutazama muvi zilizo tafsiriwa kwa kiswahili bure pamoja na chanel za azam tv na Dstv

Kiungo mchezeshaji wa Yanga, Muivory Coast Pacome Zouzoua amepanga kuwa na msimu mzuri katika msimu ujao, ikiwemo kuendelea kuipa mataji timu hiyo.

Nyota huyo ni kati ya wachezaji walitoa mchango mkubwa katika kikosi hicho, ikiwemo kutetea Ubingwa wa Ligi Kuu Bara na kuifikisha timu katika hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu huu.

Akizungumza nasi, Pacome alisema kuwa majeraha ya goti aliyoyapata katikati ya msimu huu, yameharibu mipango yake aliyoiweka.

Pacome alisema kuwa, majeraha hayo yamesababisha ashindwe kuonyesha kiwango chake bora alichonacho, akiwa na Yanga aliyojiunga nayo msimu huu.

Ipo wazi kwamba Yanga ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara wamemaliza msimu wa 2023/24 wakiwa namba moja na pointi 80 kibindoni baada ya mechi 30.


Pia, wana taji la CRDB Federation Cup ambalo walitwaa mbele ya Azam FC kwenye fainali iliyochezwa Uwanja wa New Amaan Complex.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post