Klabu ya Simba imefanya mazungumzo na wasimamizi wa mlinzi wa kimataifa wa Congo DR Nathan Fasika Idumba
Fasika kwa sasa anaitumikia klabu ya Valerenga ya Norway kwa mkopo akitokea Cape town City ya Afrika Kusini
Hii sio mara ya kwanza kwa Simba kujaribu kumsajili mchezaji huyo. Walimuwania msimu uliopita kabla ya Valerenga kufanikiwa kumsajili kwa mkopo
Simba inataka kumchukua Fasika kwa mkopo wa msimu mzima baada ya kuwa amemaliza mkataba wake na Valerenga
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali ametamba baada ya kufanikisha usajili wa Lameck Lawi kutoka klabu ya Coastal Union, kuna usajili mwingine wa beki wa Kimataifa ambao wataukamilisha siku chache zijazo
Wiki ijayo itakuwa busy kwa Simba kwani ndio wiki ya kukamilisha michakato yote ya usajili kabla ya kikosi kuelekea Misri mji wa Ismailia kwa ajili ya pre-season mwanzoni mwa Julai 2024
Post a Comment