Msanii wa Bongo Fleva na mwanachama wa Simba SC, Tunda Man amesema timu yao inapitia kipindi kigumu kwenye uwanja na ndio maana kila mtu anazungumza lake.
Amesema hata Yanga, wanaweza kuwa na matatizo lakini hayawezi kuonekana kirahisi kwa sababu wanapata matokeo uwanjani.
"Leo huwezi kuona Yanga wana tatizo hilo kwa sababu ya matokeo ambayo wanayapata kwenye pitch (uwanjani).
"Leo hata kama Yanga kuna tatizo limejificha lipo wazi na mtu analiona shabiki hawezi kuliongea kwa sasa hivi kwa sababu anajua timu inafanya vizuri. Kwa sababu 51% sisi mashabiki tunataka furaha tu. Hadi Leo nimekuwa mawanachama wa Simba nalipia Simba, nanunua jezi, naingia uwanjani kwa sababu nataka furaha" alisema Tunda Man.
BONYEZA HAPA KUTAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA UJIFUNZE MAUTUNDU YA CHUMBANI
Post a Comment