Duniani kote adui mkubwa wa talent ni injury na saikolojia . Eden Hazard akiwa Chelsea alikuwa bora sana lakini baada ya kujiunga na Madrid injury ni moja ya sababu ya kustaafu kwake mapema , mtazame Mapinduzi Balama , Hassan Dilunga na wengine
Nimekutana na maoni kuwa Pacome Zouzoua ni overrated tu lakini ni average player , well mpira ni mchezo wa wazi na kila mtu anaona kwa namna yake
Sipo hapa kuwapinga lakini naona ni mapema sana kusema haya ! Pacome ametoka kwenye injury , kwenye fainali ya jana ametumika hadi dakika 120 zinatamatika na penati yake ilisaidia kurudisha matumaini
Nna swali , hivi kweli benchi ambalo lengo namba moja ni kupata taji wangekubali kuona mchezaji yupo chini ya kiwango na bado anazima hali ya kuwa kwenye benchi una Sure boy,Farid Mussa , Musonda & Mkude ?
Hawa wachezaji ni wanajeshi na mkuu wa vikosi ni maKocha , oder ya kiongozi ndio ambayo inafuatwa bila kujali unajua nini , kuna wakati mwalimu anakutuma kazi tofauti na ilivyozoelewa [ mbinu]
Mchezaji katoka kwenye injury ,mazuri yamefutwa na kumuona wa kawaida ni mapema sana na mimi sitashiriki kwenye mkumbo huo
Post a Comment