Baada ya kudaiwa kumalizana na Joshua Mutale kutoka Zambia, mabosi wa Simba umeanza kumfuatilia kiungo mkabaji wa Rivers United, Augustine Okejepha ili atue kuiboresha timu hiyo msimu ujao.
Kiungo huyo (20), inadaiwa anaonwa ni chaguo sahihi Simba kwa ajili ya msimu ujao, japo timu mbalimbali zimeonyesha kuvutiwa naye ikiwemo, FC Ural ya Urusi inayoshiki Ligi Daraja la Kwanza.
KenGold imeanza mazungumzo na kiungo wa zamani wa timu za Lipuli, Mbeya Kwanza, Polisi Tanzania na Dodoma Jiji, Jimmy Shoji Mwaisondelo. Nyota huyo ni mchezaji huru kwa sasa hivyo kuifanya KenGold iliyopanda Ligi Kuu Bara msimu huu kuanza kuinyatia saini yake dirisha hili la usajili lililofunguliwa jana Juni 15 na litafungwa Agosti 15.
Simba iko kwenye mazungumzo ya kumpata kipa Mcameroon, Joseph Fabrice Ondoa Ebogo ili kuboresha kikosi hicho. Kipa huyo anayeichezea Nimes Olympique ya Ufaransa, anatajwa kama mbadala wa Ayoub Lakred ikiwa Simba itashindwa kumbakisha licha ya kuelezwa mazungumzo yameanza chini ya Mwekezaji na Rais wa Heshima, Mohammed Dewji ‘MO’.
Fasil Kenema ya Ethiopia imeripotiwa kutuma ofa ya zaidi ya Sh100 milioni ili kumnyakua kocha wa timu za vijana za Azam FC, Mohamed Badru. Wahebeshi wamekuwa wakimtamani Badru tangu akiwa England kabla ya kuja nchini kuzinoa Gwambina na Mtibwa Sugar zilizoshuka daraja kwa vipindi tofauti.
LICHA ya kuwepo kwa tetesi kiungo mshambuliaji wa TP Mazembe, Phillipe Kinzumbi ametua Raja Casablanca, Yanga imemkomalia baada ya kujiridhisha hajasaini kokote sasa inateta na mabosi wa Mazembe walainishe mambo na waliahidi kuwapa pesa na Kennedy Musonda.
BONYEZA HAPA KUANGALIA VIDEO ZA WAKUBWA UJIFUNZE MAUTUNDU YA KULOMBANA
Post a Comment