Klabu ya Singida Black Stars (Ihefu Fc) imetangaza kuachana rasmi na jina la IHEFU SC baada ya mchakato wa mabadiliko ya usajili wa jina la Singida Black Stars kukamilika.
Taarifa ya klabu hiyo kwa umma imebainisha kuwa kutokana na mabadiliko hayo, kuanzia sasa timu hiyo itafahamika kwa jina la Singida Black Stars SC na Makao Makuu ya Klabu yatakuwa mjini Singida.
“Mabadiliko haya ni sehemu ya maboresho muhimu yanayoendelea ndani ya klabu kuelekea maandalizi ya msimu wa mashindano 2024/2025.”
Post a Comment