Ibenge kuwapokonya Simba tonge mdomoni - EDUSPORTSTZ

Latest

Ibenge kuwapokonya Simba tonge mdomoni

Ibenge kuwapokonya Simba tonge mdomoni

Mechi za Euro 2024 zinaendelea leo usikose kuzitazama mechi zote live bure kupitia simu yako download app yetu ili kuzitazama mechi zote live bure pia kwenye app yetu kuna muvi zilizotafsiriwa kwa kiswahili pamoja na chanel za azam tv na Dstv download sasa bonyeza 👉🏻👉🏻 HAPA

N'guessan Serge Archange Pokou.

Al Hilal SC wameonyesha nia ya kutaka kumsajili N'guessan Serge Archange Pokou (23) kutoka ASEC Mimosas.

Florent Ibenge ni shabiki mkubwa wa winga huyo raia wa Ivory Coast.

Pokou anahusishwa na Simba SC lakini hakuna uongozi wa timu hiyo bado unasuasua kufanya maamuzi na hata mazungumzo.

Serge Pokou ameomba rasmi kuondoka klabuni hapo

Kiungo huyo wa Ushambuliaji anayetumia mguu wa kushoto ambaye aliwahi kuifunga Simba hapa nchini wakati timu hizo zilipokutana Ligi ya Mabingwa alisema ingawa ana ofa nyingi lakini amevutiwa na ofa ya Tanzania.

“Nina ofa nyingi ikiwemo moja ya hapo Tanzania, lakini bado sijajua wapi nitakwenda ingawa napenda kuja kufanya kazi Tanzania, kuna marafiki zangu hapo wananiambia namna ligi ya huko ilivyo na ushindani,” alisema Pokou.


“Nimewaomba viongozi wa klabu wasiniwekee ngumu katika kuondoka, nafahamu hii ni timu ambayo inapenda kuuza wachezaji wake Ulaya, napenda kwenda huko lakini nani anajua ni lini ofa kama hiyo itakuja?”

Wakati Pokou akiyasema hayo, kocha wake Jullie Chevalier alisema kiungo huyo uamuzi wa kuondoka kwake unategemea na uongozi wa klabu yao endapo timu inayomtaka itawafuata kwa kuwa bado amesalia na mwaka mmoja.

“Serge (Pokou) ni mchezaji mzuri, nadhani kama atataka kuondoka itategemea na ofa ambayo itakuja kwa uongozi wa klabu, kwa kuwa amebakiza mkataba wa mwaka mmoja hapa, ingawa sijawahi kuona viongozi wanazuia mchezaji akitaka kuondoka,” alisema Chevalier.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz