Huu hapa uamuzi wa simba kuhusu Juma mgunda
Ligi mbali mbali zitaanza muda si mrefu download app yetu kutazama mechi zote za ligi kuu tanzania bara na ulaya live bure kabisa pia ndani ya app yetu utaweza kutazama muvi zilizotafsiriwa kwa kiswahili pia utaweza kutazama chanel za azam tv buree kabisa kudownload app yetu bonyeza 👉🏻👉🏻HAPA
Kaimu Kocha Mkuu wa Simba Juma Mgunda amehakikishiwa na mabosi wa timu hiyo ataendelea kubaki katika benchi la ufundi hata ikitokea mabadiliko katika nafasi yake
Mgunda anawindwa na klabu ya Coastal Union ambayo inamuhitaji kwa ajili ya kujiimarisha kuelekea michuano ya kombe la Shirikisho msimu ujao
Wakati Simba ikiwa bado haijatangaza hatma ya benchi la ufundi, usajili unaofanyika sasa umetokana na ripoti ya makocha Abdelhak Benchikha na Mgunda ambaye ndiye aliyemaliza msimu akiwa Kocha Mkuu
Litakuwa jambo la kushangaza kama Simba itaachana na Mgunda na kuleta watu wapya katika benchi la ufundi ambao hawafahamu masuala mengi kuhusu klabu
Na pengine hii ndio sababu uongozi umeona lazima Mgunda abaki hata kama kwa nafasi ya Kocha Msaidizi ikitokea mabadiliko katika nafasi ya kocha mkuu
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amesema taarifa kuhusu benchi la ufundi itatolewa wakati wowote kabla ya kikosi kuelekea Misri wiki ijayo
Post a Comment