Hizi hapa Tetesi za usajili ndani ya klabu ya Yanga
Ligi mbali mbali zitaanza muda si mrefu download app yetu kutazama mechi zote za ligi kuu tanzania bara na ulaya live bure kabisa pia ndani ya app yetu utaweza kutazama muvi zilizotafsiriwa kwa kiswahili pia utaweza kutazama chanel za azam tv buree kabisa kudownload app yetu bonyeza 👉🏻👉🏻HAPA
Jana TFF ilitangaza kuondoa kifungo cha usajili wa ndani kwa klabu ya Yanga baada ya FiFA kuiondolea kifungo kilichotokana na madai ya mshambuliaji Lazarus Kambole. Wananchi sasa wameruhusiwa kuingiza taarifa za usajili wa wachezaji wapya kwenye mfumo
Uongozi wa Yanga umeahidi kuanzia Jumatatu taarifa zitatangazwa sambamba na mipango ya pre-season
Aidha nyota wa Yanga watatakiwa kuanza kuripoti Avic Town Jumatatu tayari kwa pre-season inayotarajiwa kufanyika nje ya nchi
Tetesi zimekuwa nyingi juu ya wachezaji ambao tayari wamemalizana na Yanga lakini uhakika ni kuwa kuanzia Jumatatu kila kitu kitakuwa hadharani
Miongoni mwa majina yanayotajwa ni pamoja na mshambuliaji George Mpole aliyemaliza mkataba na klabu ya FC Lupopo ya DR Congo
Mpole ni mchezaji wa ndani, usajili wake utakuwa maalum kuchukua nafasi ya Crispine Ngushi ambaye mkataba wake umemalizika
Aidha Yanga pia inaweza kumshusha nchini mshambuliaji Jonathan Sowah, raia wa Ghana ambaye alikuwa akiitumikia Al Nasri ya Libya
Sowah aliitumikia Medeama Fc kabla ya kutimkia Libya katika usajili wa dirisha dogo
Sowah anaweza kuchukua nafasi ya Joseph Guede ambaye mkataba wake wa miezi sita umemalizika
Guede alikuwa kwenye mipango ya kocha Miguel Gamondi lakini ni wazi mahitaji yake makubwa katika mkataba mpya yanaweza kuwa sababu ya uongozi kuamua kuachana nae
Kama kila kitu kitaenda sawa, ina maana safu ya ushambuliaji ya Yanga itakuwa na watu wa kazi kwelikweli
Kennedy Musonda, Clement Mzize bado wapo, wakiongezeka Prince Dube, George Mpole na Jonathan Sowah
Stephane Aziz Ki yupo, Pacome Zouzoua yupo, Maxi Nzengeli yupo na pengine ataongezeka yule wa bango.......!
Wananchi wanasema kwa 'mtiti' huu, kuna timu zitagoma kuingia uwanjani! Pia utakuwa aina ya usajili ambao unaakisi malengo ya Yanga ya kufanya vizuri zaidi katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao
Post a Comment