Klabu ya Simba inatajwa kukamilisha usajili wa nyota wa kwanza wa kigeni, winga Joshua Mutale kutoka klabu ya Power Dynamos ya Zambia
Simba ilituma maafisa wake nchini Zambia kwa ajili ya kukamilisha usajili huo wa winga huyo kinda mwenye umri wa miaka 22 tu
Mutale anakuwa mchezaji wa kwanza wa kigeni kusajiliwa na Simba katika dirisha hili la usajili ambalo limefunguliwa rasmi leo
Aidha taarifa za ndani zimethibitisha kuwa Simba pia imeshakamilisha usajili wa wachezaji wawili wa ndani beki Lameck Lawi kutoka Coastal Union na kiungo Yusuph Kagoma kutoka klabu ya Singida Fountain Gate ambayo kuanzia msimu ujao itafahamika kama Fountain Gate
Usajili wa Simba msimu huu unafanyika chini ya uangalizi wa tajiri mwenyewe, Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' aliyerejea katika nafasi yake ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba
BONYEZA HAPA KUANGALIA VIDEO ZA WAKUBWA UJIFUNZE MAUTUNDU YA KITANDANI
Post a Comment